Hours : Mon To Fri - 09AM - 04PM, Sunday Closed

Joining Instructions

SEHEMU A: MAELEKEZO YA MALIPO

Kila mwanafunzi anapaswa kulipa jumla ya Tsh. 1,400,000/= (Shilingi Milioni Moja laki tisa tu) ikiwa gharama za Ada na Michango chuoni kwa mwaka. MALIPO HUFANYIKA MOJA KWA MOJA CHUONI KWA KUPITIA BANKI YA NMB

JINA: MLANDIZI COLLEGE OF HEALTH      A/C. 80110042893 NMB

SEHEMU B: MAHITAJI YA MWANAFUNZI AWAPO CHUONI

Yafuatayo ni mahitaji muhimu ambayo mzazi/mlezi unapaswa kumuandalia mwanafunzi kabla ya kuanza masomo.

SARE:

Wasichana: Gauni jeupe la mikono mifupi na urefu unaopita magoti anapokuwa ameketi; magauni hayo yasiwe na ribbon/urembo viatu virefu vyenye kisigino kifupi kisichotoa sauti wakati wa kutembea sakafuni na soksi nyeupe.

Wavulana: Suruali za kitambaa cha rangi ya khaki mashati yenye rangi nyeupe yenye mikono mifupi na yasiyo na urembo. Viatu vya ngozi vyenye rangi nyeusi visivyotoa sauti wakati wa kutembea sakafuni na soksi nyeupe.

NB: Mara utakapofika chuoni utapewa mwongozo wa mavazi utazingatiwa wakati wote uwapo masomoni.

VIFAA SAIDIZI KWA AJILI YA MWANAFUNZI WA MEDICINE

  1. Kifaa cha kupimia mapigo ya moyo (Stethoscope)
  2. Kifaa cha kupimia msukumo wa Damu (BP Machine)
  3. Kifaa cha kupimia joto la mwili (Thermometer)
  4. Kifaa cha kupimia urefu (Tape measure)
  5. Patella harmma
  6. Tochi ndogo maalumu ya kupimia wagonjwa
  7. Vifaa vya kuandikia kwa mfano madftari, rula, na karamu n.k

NB: Vifaa hivi tunashauri mzazi vinunuliwe awamu ya pili hapa hapa chuo kwa gharama rafiki

itakayo kuwa imetanganzwa na makambuni yanayo husika na usambazaji wa vifaa tiba.

HOSTEL

Hostel hailipiwi ni BURE kwa mwanafunzi wa Mlandizi College of Health & Allied College. Ila matumizi ya Mwanafunzi katika Hostel (consumables) hugharamiwa na Mwanafunzi husika siyo chuo.

Matumizi ya Mwanafunzi katika Hostel ambayo hugharamiwa na Mwanafunzi husika ni pamoja na:-

  1. Chakula
  2. Umeme
  3. Maji masafi
  4. Maji taka
  5. Takataka
  6. Ulinzi
  7. Usafiri kutoka chuo hadi hostel na kurudi chuo
  8. Kitanda

Aidha, vifaa vifuatavyo ni vifaa muhimu katika ukaazi katika Hostel na ni jukumu la mwanafunzi husika kuwa navyo au kutokuwa navyo

  1. Ndoo
  2. Blanketi (duvet)
  3. Mashuka
  4. Nguo za kulalia

CLINICAL MEDICINE JOINING INSTRUCTIONS FORM

HEALTH RECORDS & INFORMATION TECHNOLOGY JOINING INSTRUCTIONS